Watu zaidi ya 6 wameuawa na wengine 92 wamejeruhiwa katika shambulizi la kigaidi dhidi ya kituo cha mafunzo cha polisi kilichoko mjini Quetta, kusini magharibi mwa Pakistan.
Polisi zaidi ya mia mbili wametekwa nyara na magaidi waliovamia chuo hicho kilichoko katika jimbo la Baluchistan.
Waziri wa mambo ya ndani wa jimbo hilo Bw Sarfraz Bugti amesema, kati ya waliouawa kwenye shambulizi hilo kuna magaidi wanne na askari wawili wa polisi, huku majeruhi wakiwa ni pamoja na walinzi wanne wa usalama.
Ofisa wa uratibu wa eneo la Quetta Bw Abdul Wahid Kakar amethibitisha kuwa majeruhi hao wamepelekwa hospitalini.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |