• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uchaguzi wa bunge waanza nchini Somalia

    (GMT+08:00) 2016-10-25 09:05:26

    Tume ya uchaguzi ya Somalia imesema, uchaguzi wa baraza la chini la bunge la Somalia umeanza, na kusema hakutakuwa na muda wa kurefusha uchaguzi huo.

    Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi ya taifa ya Somalia Bw Omar Mohamed Abdulle amesema uchaguzi huo ulioanza jumapili utaendelea hadi Novemba 10.

    Bw Abdulle amesema ushindani unatarajiwa kuwa mkali, kwani hapo awali walitarajia kuwa na wagombea wawili au watatu kwa kila nafasi, lakini idadi ya wagombea imekuwa ni kubwa zaidi ya ilivyotarajiwa.

    Habari zinasema tume ya ulinzi wa amani ya Umoja wa Afrika nchini Somalia AMISOM imetuma wana usalama zaidi kwenye majimbo ya Galmud na eneo la Shebele ya kati ili kuimarisha usalama wakati wa uchaguzi.

    Kama uchaguzi wa bunge ukimalizika kama ilivyopangwa wabunge wapya watachagua rais mpya wa Somalia Novemba 30.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako