• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uchunguzi wa ajali ya treni nchini Cameroon waanza

    (GMT+08:00) 2016-10-25 09:29:21
    Ripoti iliyotolewa na televisheni ya taifa ya Cameroon inasema kazi ya uokoaji katika ajali ya kuanguka kwa treni iliyotokea Ijumaa wiki iliyopita huko Eseka, katikati ya Cameroon imemalizika, na uchunguzi kuhusu chanzo cha ajali hiyo umeanza.

    Pia imesema waokoaji wamepata mwili mmoja wa mtoto mchanga na idadi ya vifo ikaongezeka na kufikia 80 na wengine zaidi ya 500 wamejeruhiwa.

    Jana ilitangazwa kuwa siku ya maombolezo ya taifa, bendera kwenye idara mbalimbali ndani na nje ya nchi zilipepea nusu mlingoti kuwaomboleza wahanga hao.

    Vyombo kadhaa vya habari vimesema inawezekana kuwa idara ya usafiri iliongeza mabehewa ili kupunguza msongamano wa abiria.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako