• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali ya Uingereza yapitisha mpango wa upanuzi wa uwanja wa ndege wa Heathrow

    (GMT+08:00) 2016-10-26 08:53:35

    Serikali ya Uingereza imepitsha mpango wa upanuzi wa uwanja wa ndege wa Heathrow ulioahirishwa kwa muda mrefu, na kuamua kujenga njia ya tatu ya ndege.

    Waziri Mkuu wa Uingereza Bibi Theresa May amesema, upanuzi huo ni muhimu kwa mustakbali wa uchumi wa Uingereza. Ameongeza kuwa mpango huo unaonesha kuwa baada ya kujitoa kutoka Umoja wa Ulaya, Uingereza bado itakuwa nchi ya kimataifa yenye mafanikio na iliyo wazi.

    Mara baada ya serikali kupitisha mpango huo, meya wa mji wa London Bw. Sadiq Khan amepinga uamuzi huo akisema ni kosa kwa London hata Uingereza nzima, kwa kuwa serikali imepuuza maoni ya wakazi wa London. Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza Bw. Boris Johnson pia amepinga uamuzi huo hadharani.

    Wapinzani wanaona ujenzi wa njia mpya ya ndege utasababisha bomoabomoa kubwa na gharama kubwa. Mbali na hayo ujenzi huo pia utaongeza kelele za ndege na kuongeza utoaji wa hewa ya carboni.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako