• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • IEA yasema uwezo wa dunia wa kuzalisha umeme kwa nishati endelevu umepita ule wa mafuta

    (GMT+08:00) 2016-10-27 17:56:58

    Ripoti mpya iliyotolewa na Shirika la Nishati la Kimataifa IEA imesema, mwaka jana nishati endelevu zilipiku mafuta na kuhesabiwa kwa zaidi ya nusu ya ongezeko la uwezo wa kuzalisha umeme

    Ripoti hiyo inasema nusu milioni ya paneli za umeme wa jua zilifungwa kwa siku mwaka jana kote duniani, huku hapa China kila saa mitambo miwili ya umeme wa upepo ikijengwa. Ripoti hiyo pia imesema China inaendelea kuongoza duniani kutokana na upanuzi wa nishati endelevu, ikiwakilisha asilimia 40 ya ongezeko hilo.

    Nishati endelevu kama vile upepo, jua na maji zimechukuliwa kama njia muhimu katika juhudi za kimataifa za kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa, na katika nchi nyingi haswa za Asia, nishati endelevu pia ni muhimu katika kudhibiti uchafuzi wa hewa, kuongeza aina za nishati na kuongeza usalama wa nishati.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako