• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Meli ya Biashara ya China yajiunga kwenye msako wa baharia wa China aliyepotea baharini

    (GMT+08:00) 2016-10-30 18:57:50
    Meli ya biashara ya China imejiunga kwenye msako wa baharia Guo Chuan ambaye amepotea kwa takriban siku tano wakati akiwa kwenye safari ya peke yake katika bahari ya Pacific.

    Meli hiyo ijulikanayo kama Ruian City kutoka Kundi la Meli la COSCO, ilipokea ujumbe wa kuomba usaidizi jana wakati ikiwa kwenye safari zake za kawaida kati ya Hawaii na Japan.

    Kutokana na ombi hilo, maeneo mengine matano ya msako yameongezwa wakati meli hiyo tayari imeshatafuta kwenye maeneo kadhaa ambayo baharia huyo mwenye miaka 51 anaweza kuchukuliwa na maji. Guo anadhaniwa kuanguka kutoka kwenye chombo chake Oktoba 25, umbali wa kilomita 900 nje ya Hawaii na timu yake imesema inawezekana amevaa koti la kujiokolea.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako