• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tetemeko la ardhi lenye nguvu ya 6.5 latokea katikati ya Italia

    (GMT+08:00) 2016-10-31 09:52:24

    Taarifa iliyotolewa na taasisi ya utafiti wa volkano ya Italia imesema tetemeko la ardhi lenye nguvu ya 6.5 kwenye kipimo cha Richter lilitokea jana kwenye sehemu ya kati ya Italia.

    Kiini cha tetemeko hilo kiko kwenye kina cha kilomita 10 chini cha ardhi kwenye mpaka wa mikoa ya Macerata na Perugia.

    Watu kadhaa wamejeruhiwa huku majengo mengi yakibomoka katika totomeko hilo. Majengo mengi yaliyobomoka yako kwenye miji mdogo iliyo karibu na kiini cha tetemeko, na baadhi yao yana thamani kubwa ya kihistoria.

    Tetemeko hilo ni la nne kutokea katika miezi miwili iliyopita, na pia ni tetemeko lenye nguvu zaidi nchini humo tangu mwaka 1980.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako