• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Magufuli awasili Kenya kwa ziara rasmi ya siku mbili

    (GMT+08:00) 2016-11-01 09:56:49

    Rais wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli amepuuzilia mbali madai kwamba serikali yake imekuwa ikijitenga na majirani zake na kufanya mambo yake bila ushirikiano na nchi jirani.

    Rais Magufuli aliyasema haya jana katika ziara yake ya kwanza nchini Kenya tangu achaguliwe kuwa rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania.

    Rais wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli ambae yuko nchini Kenya kwa ziara rasmi amesema yuko nchini Kenya kwa ajili ya kuimarisha uhusiano mzuri ambao umekuwa tangu kitambo baina ya nchi hizi mbili.

    Magufuli amesema kuwa mara kwa mara yeye na mwenyeji wake Rais Uhuru Kenyatta huwa wanaongea kwa simu ,jambo ambalo huwa halizungumzwi katika vyombo vya habari.Hivyo alitoa hakikisho kwamba amekuwa akiwasiliana na Rais Kenyatta na wamekuwa wakijadiliana kuhusu mambo mbalimbali.

    Dkt Magufuli ambaye uongozi wake umepongezwa na wengi baada ya kupigana na rushwa,alisema yuko Nairobi ili kueleza kuhusu sera zake ambazo zinaifanya Tanzania kuwa sehemu nzuri ya uwekezaji.

    Aidha Magufuli alisema kwamba amemhakikishia Rais Kenyatta kwamba Kenya mwenza nambari moja wa kibiashara wa Tanzania,na kueleza kuwa kuna makampuni mengi ya Kenya nchini Tanzania kuliko taifa lolote la Afrika.

    Alisema Tanzania inawakaribisha wakenya wote ambao wanataka kufanya biashara jijini Dar es Salaam.

    Kwa upande wake Rais Uhuru Kenyatta alisema Kenya na Tanzania zimekuwa na uhusiano mwema tangu miaka ya kitambo.

    Aidha Kenyatta alisema kuwa Kenya na Tanzania ni baadhi ya nchi chache za Afrika ambazo zimekuwa na mabadiliko ya serikali kwa njia ya demokrasia na amani.

    Rais Uhuru Kenyatta alisema Mawaziri wan chi za nje wa Kenya na Tanzania watapanga kamisheni ya pamoja ambayo itakutana nchini Tanzania hivi karibuni na kupanga utekelezaji wa kazi ambazo serikali hizo mbili zitakuwa zinafanya.

    Pia alisema walijadiliana kuhusu matatizo ya nchi za Afrika mashariki.

    INSERT

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako