• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Vikosi vya Iraq vyaanza operesheni mpya kuingia mjini Mosul

    (GMT+08:00) 2016-11-01 10:01:54

    Vikosi vya usalama vya Iraq vimesogea karibu na kingo za mji wa Mosul kwenye operesheni mpya ya kijeshi yenye lengo la kuwafukuza wapiganaji wa kundi la IS kutoka mji huo.

    Baada ya mapambano ya saa kadhaa, vikosi vya usalama vya Iraq vimekomboa vijiji kadhaa vilivyo karibu na mji wa Mosul.

    Taarifa iliyotolewa mapema siku hiyo inasema, jeshi la Iraq na vikosi vya kupambana na ugaidi vilianza operesheni mpya asubuhi mapema, na kuelekea kando ya Mashariki ya Mto Tigris unaopita mji huo kwa njia tatu.

    Katika wiki mbili zilizopita vikosi vya Iraq vilifanya mashambulizi ya mizinga dhidi ya vituo vya IS kwenye eneo la viwanda nje ya Mosul, huku ndege za Iraq na washirika zikifanya mashambilizi dhidi ya shabaha ndani ya nje ya mji huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako