• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Viongozi wa Kenya na Tanzania wazindua ujenzi wa barabara iliyojengwa na China huko Nairobi

    (GMT+08:00) 2016-11-02 09:24:19

    Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya na rais John Pombe Magufuli wa Tanzania, jana walishiriki kwenye uzinduzi wa barabara iliyoko kusini mwa Nairobi, Kenya.

    Asilimia 85 ya fedha za ujenzi wa barabara hiyo zimetolewa na benki ya Exim ya China, na ujenzi wake ulitekelezwa na Kampuni ya China ambayo pia inashughulikia ujenzi wa reli kati ya Nairobi na Mombasa.

    Akihutubia kwenye sherehe hiyo, rais Kenyatta amesema barabara hiyo yenye umbali wa kilomita 28 inaunganisha barabara kuu mbili, na itasaidia kuondoa msongamano wa magari barabarani mjini Nairobi.

    Rais Magufuli ambaye pia ni mwenyekiti wa zamu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki amepongeza mchango wa China katika maendeleo ya miundo mbinu kwenye kanda hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako