• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mjumbe wa Umoja wa Mataifa kwenye nchi za Maziwa Makuu ataka eneo la Maziwa Makuu lipatiwe uungaji mkono zaidi

    (GMT+08:00) 2016-11-03 08:45:05

    Mjumbe maalum wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa kwenye eneo la Maziwa Makuu Bw Said Djinnit, ametoa mwito wa kutolewa uungaji mkono zaidi wa kimataifa kwa eneo la Maziwa Makuu.

    Bw Djinnit amesema eneo hilo bado linakabiliwa na changamoto kubwa ikiwa ni pamoja na uwepo wa makundi ya waasi kwenye eneo la mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo. Amesema uungaji mkono kwa Burundi na Jamhuri ya Afrika ya Kati ni muhimu, kutokana na matukio yanayohusiana na uchaguzi na makundi yenye silaha, yanafanya hali ya eneo hilo iendelee kuwa tete.

    Bw Djinnit ambaye amepongeza ushirikiano kati ya jeshi la Umoja wa Mataifa na jeshi la serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), ameonyesha wasiwasi kuhusu uwepo wa wapiganaji wa kundi la upinzani la Sudan Kusini SPLM, kwenye eneo la mashariki mwa DRC.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako