• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mawaziri wakuu wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai wakutana nchini Kyrgyzstan

    (GMT+08:00) 2016-11-03 20:10:42

    Mkutano wa 15 wa ngazi ya mawaziri wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai SCO umeanza leo mjini Bishkek, mji mkuu wa Kyrgyzstan, kwa lengo la kuongeza maingiliano zaidi kati ya nchi wanachama.

    Kwenye mkutano huo, waziri mkuu wa China Li Keqiang akizungumzia ushirikiano kati ya nchi wanachama wa SCO katika siku zijazo, ametoa mapendekezo sita yaani kuhakikisha mazingira yenye usalama na utulivu, kuunganisha mikakati ya maendeleo, kuinua kiwango cha ushirikiano wa uzalishaji viwandani, kutafuta fursa za ushirikiano katika kuhimiza uvumbuzi, kukamilisha utaratibu wa kikanda wa ukusanyaji fedha, na kuimarisha msingi wa mawasiliano ya kiutamaduni.

    Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo, kaimu waziri mkuu wa Kyrgyzstan Sooronbay Zheenbekov amesifia ushirikiano ndani ya Jumuiya hiyo katika miaka 15 iliyopita, na kuahidi kuboresha hatua zaidi za ushirikiano katika maeneo kadhaa. Amesema nchi wanachama wa Jumuiya hiyo zimepata matokeo dhahiri katika nyanja zote, na katika siku zijazo, nchi hizo zitaendeleza zaidi uhusiano na ushirikiano katika mambo ya uchumi, biashara, usalama na utamaduni.

    Amesema pendekezo la Ukanda Mmoja na Njia Moja lililotolewa na China ni la muhimu zaidi na Jumuiya hiyo itatafuta kuchukua nafasi kubwa zaidi katika utekelezaji wake.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako