• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mradi wa umwagiliaji maji kaunti ya West Pokot wazinduliwa

    (GMT+08:00) 2016-11-04 10:30:47

    Rais Uhuru Kenyatta amezindua awamu ya tatu ya mradi wa umwagiliaji maji wa Sigor WeiWei, katika kaunti ya West Pokot. Mradi huu utafadhiliwa na Serikali ya Italia kwa kushirikiana na Mamlaka ya maendeleo ya bonde la Kerio (KVDA) na inakadiriwa kugharimu shilingi bilioni moja za Kenya.

    Rais Kenyatta amesema serikali iko mbioni kupambana na umaskini na kurudisha amani katika eneo la bonde la Kerio kupitia mradi huo.

    Akizungumza na wananchi katika shamba la Wei Wei Sigor baada ya uzinduzi wa mradi, Rais Kenyatta amesema mradi huo sio tu utaongeza usalama wa chakula kwenye eneo hilo pekee bali kwa nchi nzima.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako