• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • UN yapongeza kuanza kufanya kazi rasmi kwa makubaliano ya Paris

    (GMT+08:00) 2016-11-05 18:09:39

    Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amepongeza kuanza kufanya kazi rasmi kwa makubaliano ya mabadiliko ya hali ya hewa ya Paris.

    Bw. Ban amesema, mkutano wa 22 wa wajumbe wa azimio la mfumo wa kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa wa Umoja wa Mataifa utafanyika tarehe 7 mwezi huu mjini, Marrakech, Morocco. Hata hivyo amesema tatizo linalowakabili kwa sasa ni kudumisha mwelekeo mzuri wa kusukuma mbele utekelezaji wa makubaliano hayo. Na kuitaka jamii ya kimataifa kuwa na nia wa kudumu ya kufuata njia ya kisayansi na kuitumia fursa hiyo kujenga dunia yenye usalama zaidi na maendeleo endelevu.

    Rais wa Baraza kuu la 71 la Umoja wa Mataifa Peter Thomsen amesema, kufanya kazi rasmi kwa makubaliano ya Paris kunaleta matumaini ya kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa.

    Naye msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bibi Hua Chunying amesema, China inapongeza kuanza kufanya kazi rasmi kwa makubaliano hayo ndani ya mwaka mmoja tangu kupitishwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako