• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Messi, Suarez watupia 2 La Liga, Arsenal yalazimishwa sare na Tottenham

    (GMT+08:00) 2016-11-07 09:02:24

    Nyota wa Barcelona, Lionel Messi na Luis Suarez wameifungia timu yao ya Barcelona na kuibuka ushindi wa goli 2-1 dhidi ya Sevilla kwenye mchezo wa La Liga uliochezwa katika uwanja wa Sanchez Pizjuan. Bao la Sevilla limefungwa na Vitolo.

    Huko Uingereza, mchezaji Harry Kane ameweza kuisawazishia timu yake Tottenham dhidi ya wenyeji Arsenal katika mchezo uliochezwa uwanja wa Emirates.

    Kane alifunga kwa njia ya penati mapema kipindi cha pili, huku goli la Arsenal lilipatikana baada ya Kevin Wimmer kujifunga dakika tatu kabla ya kipindi cha mapumziko.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako