• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wamarekani wanapiga kura kumchagua rais wao mpya

    (GMT+08:00) 2016-11-08 19:59:03

    Wamarekani wanaelekea kwenye vituo mbalimbali vya kupigia kura kote nchini humo ili kumchagua rais wao mpya.

    Zoezi hili lilianza rasmi baada ya watu wa vijiji vitatu vya jimbo la New Hamsphire mashariki mwa Marekani kupiga kura zao.

    Kuhusiana na uchaguzi huo, hivi karibuni mke wa mgombea urais kupitia chama cha Republican Donald Trump Bi. Melanie Trump alizungumza kwenye kampeni za mumewe na kusema, anachokipinga Trump ni wahamiaji haramu, lakini anaunga mkono wahamiaji halali. Bi. Melanie amesema hayo kutokana na jamii kuelewa kuwa Trump anapinga wahamiaji.

    Wataalam wanasema, Trump alipaswa kufanya hayo mapema zaidi na sio dakika za mwisho, ambapo baadhi ya watu tayari wameshapiga kura zao mapema. Wataalam hao wanasema Trump anaponzwa na kauli zake alizokuwa akizitoa dhidi ya udhalilishaji wa wanawake na baadhi ya jamii zenye watu wachache, na badala yake alipaswa kuzungumzia zaidi masuala muhimu kama uchumi na ajira, mambo ambayo Wamarekani wengi wanayafuatilia katika uchaguzi wa mwaka huu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako