Mwandaaji wa mkutano huo Bw. Schuyler Thorup amesema mkutano huo una lengo la kuweka mpango wa kuhimiza maendeleo ya kazi kuhusu lishe, maji na usafi, kilimo, afya, maendeleo ya utotoni, elimu na jinsia.
Bw Thorup amesema kila mwaka utapiamlo husababisha vifo vya watoto takriban milioni 3 wenye umri chini ya miaka mitano, na kuleta hasara ya mabilioni ya pesa kwa uchumi wa dunia.
Wawakilishi wa mashirika mbalimbali ya kibinadamu kama UNICEF na WFP wanatarajiwa kushiriki kwenye mkutano huo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |