• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Semina ya ushirikiano kuhusu viwanda na kilimo kati ya China na Afrika yafanyika Afrika Kusini

    (GMT+08:00) 2016-11-10 19:39:51

    Semina ya ushirikiano kuhusu maendeleo ya viwanda na kilimo cha kisasa kati ya China na Afrika imefanyika mjini Pretoria, Afrika Kusini.

    Akizungumza kwenye semina hiyo, balozi wa China nchini Afrika Kusini Tian Xuejun amesema, maendeleo ya viwanda na kilimo cha kisasa vimepewa kipaumbele katika mipango kumi ya ushirikiano iliyotangazwa na rais Xi Jinping wa China kwenye mkutano wa kilele wa FOCAC uliofanyika mwishoni mwa mwaka jana mjini Johannesburg. Anatarajia kuwa washiriki wa semina hiyo watatoa mapendekezo yanayotekelezeka ya kuhimiza mafanikio yaliyofikiwa kwenye mkutano huo na kuimarisha ushirikiano kati ya China na Afrika.

    Kwa upande wake, naibu waziri wa ikulu ya Afrika Kusini Buti Manamela amesema, hivi sasa, Afrika Kusini inatekeleza mpango wa maendeleo ya taifa. Anatoa mwito kwa China na Afrika Kusini kuendelea na ushirikiano wa kunufanishana, kusukuma mbele maendeleo yasiyochafua mazingira na endelevu, kushirikiana katika kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa na kusaidia Afrika kuandaa wataalamu zaidi katika ulinzi wa mazingira.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako