• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China apongeza kufanyika kwa kongamano la kimataifa la majumba ya makumbusho

    (GMT+08:00) 2016-11-10 19:41:09

    Rais Xi Jinping wa China amepongeza kufunguliwa kwa kongamano la kimataifa kuhusu majumba ya makumbusho lililoanza leo mjini Shenzhen, China.

    Rais Xi amesema, majumba ya makumbusho ni sehemu muhimu zinazohifadhi na kurithi ustaarabu wa binadamu, pia ni madaraja yanayounganisha siku za zamani, sasa na baadaye. Amesema majumba hayo yanafanya kazi za kipekee katika kuhimiza kuwasiliana na kujifunza kuhusu ustaarabu wa dunia. Pia amesema katika miaka ya karibuni, majumba ya makumbusho ya China yamepata maendeleo katika ujenzi wa vifaa, uhifadhi na utafiti wa makusanyo na kusukuma mbele mawasiliano ya kitamaduni kati ya China na nchi nyingine.

    Ametoa mwito kwa washiriki wa kongamano hilo kutumia busara katika kuendesha majumba ya makumbusho na kutoa mchango katika kulinda aina tofauti za tamaduni, kuongeza maelewano miongoni mwa watu wa nchi mbalimbali na kuhimiza maendeleo ya ustaarabu wa binadamu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako