• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yapenda kushirikiana na serikali mpya ya Marekani kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa

    (GMT+08:00) 2016-11-10 20:30:46

    Afisa wa China anayeshughulikia masuala ya mabadiliko ya hali ya hewa amesema China inapenda kushirikiana na Marekani katika kukabiliana na mabadiliko hayo.

    Naibu kiongozi wa ujumbe wa China kwenye mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa unaofanyika huko Marrakech, Morocco, Gou Haibo amesema hayo baada ya Donald Trump kuchaguliwa kuwa rais wa Marekani. Wakati wa kampeni za uchaguzi zilizofanyika nchini humo, Bw. Trump alisema anatafakari kutengua mpango wa utekelezaji wa serikali ya Obama kuhusu kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa na kujitoa kwenye Makubaliano ya Paris.

    Bw. Gou amesema, China ina msimamo imara wa kuhimiza ushirikiano na pande nyingine katika kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa.

    Anasema, "Maendeleo yasiyochafua mazingira ni mkondo mkuu wa dunia yetu, uaratibu wa kimataifa wa kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa uliomo kwenye Makubaliano ya Paris unalingana na mkondo huu na pia maslahi ya nchi mbalimbali na jamii ya kimataifa. China ikiwa nchi kubwa zaidi inayoendelea, inashikilia njia za maendeleo za uvumbuzi, uratibu, uwazi na kunufaishana, kushikilia utaratibu wa kimataifa wa kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa na kushikilia kuhimiza ushirikiano wa kimataifa."

    Bw. Gou ameongeza kuwa China imefanya kazi zake vizuri, na inapenda kufanya juhudi na pande nyingine ikiwemo Marekani kuhimiza utaratibu na ushirikiano husika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako