• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Obama na Bw Trump wakutana na kujadili mambo mengi kwenye mkutano wao wa kwanza baada ya uchaguzi

    (GMT+08:00) 2016-11-11 09:04:40

    Rais Barack Obama wa Marekani na Rais mteule Donald Trump wamekutana kwa mara ya kwanza tangu Bw Trump achaguliwa kuwa Rais wa Marekani.

    Rais Obama amesema jambo la kipaumbele katika miezi miwili ijayo ni kufanikisha makabidhiano ya urais na kuhakikisha kuwa Rais mteule Bw Trump anakuwa na mafanikio.

    Wakati jamii ya Marekani inaonekana kuwa na mgawanyiko mkubwa kwenye uchaguzi mkuu, Rais Obama amesema ni muhimu kwa wamarekani wote kuungana, na kukabiliana na changamoto zinazoikabili Marekani. Pia amesema pamoja na kuwa yeye ana tofauti na Bw Trump, anaamini kuwa ni muhimu kuhakikisha mpito unakuwa wa amani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako