• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yataka madaraka wanayopewa polisi wa kulinda amani yawe ya uwazi na kutekelezeka

    (GMT+08:00) 2016-11-11 18:20:09

    Naibu balozi wa China katika Umoja wa Mataifa Bw. Wu Haitao amesema, madaraka wanayopewa polisi wa kulinda amani yanatakiwa kufuata mahitaji na hali halisi ya nchi wanazopelekwa na ya nchi zinazowapeleka, pia yanapaswa kurekebishwa kuendana na mabadiliko ya mazingira ili kutimiza malengo ya operesheni za kulinda amani.

    Akishiriki kwenye mkutano wa Baraza la Usalama kuhusu askari wa kulinda amani, Bw. Wu amesema, ni lazima kuheshimu mamlaka ya nchi wanazokwenda polisi hao, kusikiliza maoni yao na kuongeza mawasiliano na nchi hizo kuhusu muda wa operesheni na marekebisho ya madaraka yao. Pia amesema, China ni nchi inayopeleka kwa wingi zaidi askari wa kulinda amani kati ya nchi wajumbe wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

    Ameongeza kuwa China inapenda kushirikiana na jumuiya ya kimataifa kujitahidi kutoa mchango katika maendeleo ya shughuli za kulinda amani za Umoja wa Mataifa na kulinda amani na utulivu wa kimataifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako