• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Vifo vinavyotokana na ugonjwa wa surua duniani vyapungua

    (GMT+08:00) 2016-11-11 18:40:17

    Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF),Shirika la Afya Duniani (WHO), na Shirika la Kimataifa la Chanjo (GAVI) zimetoa ripoti ya pamoja ikisema, idadi ya vifo vinavyotokana na ugonjwa wa surua duniani imepungua kwa asilimia 79 kutoka mwaka 2000 hadi mwaka 2015, lakini maendeleo ya kuondoa tishio la ugonjwa huo hayana uwiano.

    Ripoti hiyo inasema, katika miaka 15 iliyopita, mpango wa kutoa chanjo ya surua katika maeneo makubwa umeokoa watoto milioni 20, lakini mwaka jana, idadi kama hiyo ya watoto walikosa chanjo hiyo, ambao nusu yao wanatoka nchi za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Ethiopia, India, Indonesia, Nigeria na Pakistan, na idadi ya vifo vinavyotokana na ugonjwa wa surua katika nchi hizo inachukua asilimia 75 ya ile ya dunia nzima.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako