Bw Keating amesema ahadi zilizotolewa na Rais Abdiweli Mohamed Ali "Gaas" wa Puntland, na Abdikadir Hussein Guled wa Galmudug yanaridhisha, lakini ni lazima ziendane na utekelezaji kamili wa makubaliano.
Taarifa ya Bw Keating inakuja baada ya mazungumzo yaliyofanyika mjini Galkayo na kuhudhuriwa na viongozi wa Somalia ikiwa pamoja na waziri mkuu wake Bw. Sharmarke, wawakilishi wa jumuiya ya kimataifa, wakuu wa majimbo hayo mawili.
Mapambano yaliyolipuka mjini Galkayo yamesababisha vifo vya watu 45 katika muda wa wiki sita, na kufanya watu elfu 90 kupoteza makazi yao.
.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |