• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mabingwa wa NBA waenda ikulu kumuaga Obama

    (GMT+08:00) 2016-11-14 09:17:46

    Staa wa kikapu nchini Marekani katika Ligi ya NBA, LeBron James ameiongoza timu yake ya Cleveland Cavaliers kutembelea ikulu ya nchi hiyo kutokana na kutwaa ubingwa NBA msimu uliopita.

    Wakiwa ikulu wachezaji wa timu hiyo walijumuika na aliyekuwa rais wa nchi hiyo, Barrack Obama na mkewe, Michelle Obama ikiwa pia ni sehemu ya kumuaga kuondoka madarakani kumpisha Donald Trump ambaye amechaguliwa katika uchaguzi wa rais uliofanyika wiki iliyopita.

    Imekuwa ni kawaida timu inaposhinda NBA kupata nafasi ya kwenda kutembelea mjengoni hapo maarufu kwa jina White House.

    Katika hotuba yake aliyoitoa kwa wachezaji hao, Obama amemsifia James kwa kuonyesha uwezo wa juu na kueleza kuwa ni mchezaji ambaye hana ubinafsi anapenda mafanikio ya wengi, anajituma na ana nidhamu ya kazi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako