• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jeshi la Somalia latwaa tena vijiji kutoka kwa kundi la Al-Shabaab

    (GMT+08:00) 2016-11-14 09:49:01

    Jeshi la taifa la Somalia linaloungwa mkono na jeshi la Umoja wa Afrika limetwaa tena udhibiti wa vijiji vya El-Garas huko Bakool, kusini magharibi mwa Somalia kutoka kwa kundi la Al-Shabaab.

    Waziri wa habari wa jimbo la magharibi kusini mwa Somalia Bw. Ugas Hassan amesema kuwa operesheni inaendelea ili kutwaa maeneo zaidi yanayodhibitiwa na kundi hilo, ukiwemo mji wa Tiyeglow, ambao uliachwa na jeshi la Ethiopia mwezi Oktoba.

    Amesisitiza kuwa jimbo la Kusini Magharibi mwa Somalia halitavumilia vitendo vya kikatili vinavyofanywa na wapiganaji wa kundi la Al Shabaab dhidi ya wakazi wa huko.

    Hatua iliyochukuliwa na jeshi la Somalia inafuatia mauaji ya watu watano yaliyofanywa na wapiganaji wa kundi la Al Shabaab katika mji wa Tiyeglow.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako