• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yatazamiwa kutimiza lengo la ongezeko la uchumi la zaidi ya asilimia 6.5

    (GMT+08:00) 2016-11-14 18:39:24

     

    Idara ya takwimu ya China imetangaza takwimu mpya kuhusu faida za viwanda, uwekezaji wa mali za kudumu, uendelezaji, uwekezaji, na mauzo ya mali zisizohamishika. Ofisa wa idara hiyo amekadiria kuwa uchumi wa China unatazamiwa kutimiza lengo la ongezeko la uchumi la zaidi ya asilimia 6.5.

    Kwa mujibu wa takwimu hizo, mwezi Oktoba thamani ya ongezeko la viwanda ambavyo pato la uendeshaji limezidi RMB yuan milioni 20 kwa mwaka imeongezeka kwa asilimia 6.1, ongezeko hili ni asilimia 0.5 kuliko mwaka jana wakati kama huu, na thamani ya jumla ya mauzo ya rejareja ya bidhaa za kijamii ilifikia trilioni 3.1, ambalo ni ongezeko la asilimia 10 kuliko mwaka jana.

    Mbali na hayo, katika miezi kumi iliyopita, uwekezaji wa mali zisizohamishika nchini China ulifikia RMB yuan laki 4.84, hili ni ongezeko la asilimia 8.3 kuliko mwaka jana; thamani ya jumla ya uwekezaji katika sekta za utoaji wa huduma iliongoza sekta nyingine; huku ongezeko la uwekezaji wa uendelezaji wa mali zisizohamishika likipungua.

    Kati ya uwekezaji katika sekta mbalimbali, uwekezaji usio wa kiserikali umeongezeka kwa miezi miwili mfululizo. Bw. Mao Shengyong akizungumzia hali hiyo anasema:

    "Uwekezaji usio wa kiserikali uliongezeka kwa asilimia 2.9 kati ya mwezi Januari hadi Oktoba. Hili ni ongezeko la asilimia 0.4 kuliko miezi tisa iliyopita. Hali hii imeonesha kuwa mahitaji ya soko yanaongezeka."

    Msemaji huyo amesema uchumi wa China umedumisha mwelekeo wa kupata maendeleo kwa hatua madhubuti, huku kiwango cha watu wasio na ajira katika miji mikubwa kikidumisha kiwango cha chini ya asilimia 5. Mtafiti wa Taasisi ya utafiti wa maendeleo ya Baraza la serikali la China Bw. Zhang Liqun amesema, mabadiliko ya vigezo muhimu vya uchumi kwa mwezi Oktoba yameonesha kuwa, mwelekeo wa uchumi wa China wa kupata maendeleo haubadiliki, anasema:

    "Kutokana na takwimu za mwezi Oktoba, kiwango cha jumla cha manunuzi kimekuwa kikiongezeka kwa hatua madhubuti, huku mwendo wa ongezeko la uwekezaji ukidumishwa kwa kupanda, hali ambayo imeonesha kuwa mahitaji katika soko la ndani nchini China yanaongezeka kwa hatua madhubuti."

    Bw. Mao Shengyong amekadiria kuwa, mwelekeo wa uchumi wa China wa kuongezeka kwa hatua madhubuti hautabadilika katika miezi mitatu ya mwisho ya mwaka huu, na hakutakuwa na matatizo katika kutimiza lengo la ongezeko la uchumi la kati ya asilimia 6.5 hadi 7.0 kwa mwaka huu. Pia ameeleza kuwa, hivi sasa uchumi wa China unakabiliwa na changamoto fulani, mazingira ya kimataifa na ya ndani bado yana utatanishi, na msingi wa kutimiza ongezeko la kudumu la uchumi bado si thabiti. Katika siku zijazo China itaendelea kuongeza nguvu katika kutekeleza kazi mbalimbali, ili kuhakikisha uchumi unapata maendeleo kwa hatua madhubuti.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako