• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: Bett amewataka wakulima wadogo kujitosa katika kilimo cha pamba

    (GMT+08:00) 2016-11-14 21:10:47

    Waziri wa Kilimo Willy Bett, amewataka wakulima wadogo kujitosa katika kilimo cha pamba ili kusaidia kufufua sekta hiyo.

    Kumekuwa na uzalishaji wa chini wa pamba nchini. Hivi sasa Kenya inazalisha tani 4000 za pamba, dhidi ya mahitaji ya tani 10,000.

    Bett ambaye alizungumza katika kaunti ya Kwale wiki iliyopita wakati wa ziara ya mradi wa kilimo cha pamba alisema kupanda kwa pembejeo kumechangia changamoto zinazokabili sekta hiyo.

    Amasema hii, imefanya sekta ya pamba kutokuwa na ushindani katika masoko ya ndani na kimataifa.

    Aidha amesema serikali imeweka kanuni na sera, kuhakikisha pamba inaimarishwa.

    Amesema Kenya inaagiza zaidi ya asilimia 50 ya pamba,ambayo baadaya inaweka shinikizo juu mahitaji ya fedha za kigeni.

    Ripoti ya Benki ya Dunia mwaka wa (2005) ilionyesha mambo ambayo yanachangia kudorora kwa sekta ya pamba, ukame wa mara kwa mara, kubadilika kwa bei ya uzalishaji, malipo ya wakulima kuchelewa na ukosefu wa upatikanaji wa mbegu bora.

    Kampuni yua Titanium imeanzisha mapngo wa kilimo cha pamba na wakazi wa kwale ili kusaidia kuboresha hali ya maisha.

    Hivi sasa kampuni hiyo inalenga wakulima 1,500 kufanya kilimo hicho katika msimu ujao.

    Serikali imetoa sh bilioni 1 katika kipindi cha miaka miwili iliyopita ya fedha ya kuboresha kampuni ya nguo miller Rivatex inayomilikiwa na serikali mjini Eldoret.

    Mwezi Machi mwaka huu, mradi huu ulipokea ufadhili wa Sh bilioni 3 kutoka serikali ya India kwa ajili ya ununuzi wa mashine mpya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako