• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jeshi la Iraq lawaua wapiganaji wasiopungua 57 wa kundi la Islamic State huko Mosul

    (GMT+08:00) 2016-11-15 09:53:51

    Jeshi la Iraq limewaua wapiganaji wasiopungua 57 wa kundi la Islamic State ndani na karibu mji wa Mosul, na mapambano dhidi ya wapiganaji hao yanaendelea.

    Makamando wa kikosi cha kupambana na ugaidi walizuia mashambulizi mengi ya kujitoa mhanga ya wapiganaji wa kundi la Islamic State kwenye sehemu zilizokombolewa mashariki mwa Mosul, zikiwemo al-Qadsiyah na Zahraa.

    Kasi ya kuukomboa mji wa Mosul kutoka kwa wapiganaji wa kundi la IS imepungua, kutokana na kundi hilo kutumia vikundi vidogo vya wapiganaji wenye ujuzi mkubwa na kusaidiwa na wadunguaji, washambuliaji wa kujitoa mhanga, na mabomu ya kutegwa ardhini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako