• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kongamano la awamu ya 27 la sayansi katika nchi zinazoendelea lafunguliwa huko Kigali, Rwanda

    (GMT+08:00) 2016-11-15 09:59:27

    Rais Paul Kagame wa Rwanda amefungua rasmi kongamano la awamu ya 27 la sayansi katika nchi zinazoendelea jijini Kigali Rwanda.

    Kongamano hili la siku nne linalenga kutafuta suluhisho la changamoto za baa la njaa,magonjwa na umaskini kupitia kwa ubunifu wa sayansi pamoja na kutuza wanasayansi waliofanya miradi ya maendeleo katika nchi zinazoendelea.

    Rais wa taasisi ya kimataifa ya sayansi Profesa Bai Chunli kutoka China amesema licha ya changamoto nyingi zinazokumba nchi za Afrika,utafiti wa hivi karibuni unaonyesha wanasayansi wamefanikiwa kufanya uvumbuzi uliotoa suluhu la matatizo ya jamii kupitia sayansi.

    Profesa Bai amesema kongamano hili limefanyika Rwanda mwaka huu kutokana na juhudi zao za kuwekeza raslimali na bidii nyingi katika ushirikiano wa kuboresha sayansi na uvumbuzi Afrika.

    China imetia sahihi mkataba wa makubaliano ya ushirikiano wa kukuza sayansi nchini Rwanda na Afrika .

    Kwa mujibu wa mkataba huo,China imetoa fursa kwa wanafunzi 100 wa vyuo vikuu vya sayansi kupokea masomo ya juu kwa ufadhili wa serikali.

    Imebainika kwamba ,idadi ya wanasayansi katika bara la Afrika bado ni kidogo hivyo takriban wanasayansi milioni 1 wanahitajika katika mda wa miaka 10 ijayo.

    ' China itaendelea kufungua fursa kwa wanasayansi wadogo kujiendeleza kwani zaidi ya wanasayansi milioni moja wanahitajika katika mda wa miaka 20 ijayo"

    Kutokana na harakati za Rwanda za sayansi,China aidha imekubali kuanzisha kituo cha taasisi ya utafiti wa sayansi nchini Rwanda itakayotoa nafasi kwa wanasayansi wadogo kuelimika zaidi.

    Rais Paul Kagame wa Rwanda amesisitiza umuhimu wa sayansi katika kubadilisha jamii na uchumi na kuwapongeza washindi kutoka nchi tofauti waliotambuliwa kutokana mchango wao kwenye sayansi ulioleta mabadiliko makubwa.

    " Sayansi ni sekta muhimu sana katika maendeleo ya Afrika.Nchini Rwanda na Afrika wanasayansi wamechangia pakubwa kwa ustawi wa uchumi mazingira na kilimo.Sayansi imefanikiwa kutoa suluhisho kwa matatizo ya afrika na imechangia katika ukuwaji wa uchumi."

    Amesema Afrika itaendelea kushirikiana na waliobobea kwenye sekta hii ili kumaliza changamoto za maisha.

    Waziri wa elimu na sayansi nchini Rwanda Patia msafiri amepongeza msaada wa China katika sayansi nchini Rwanda na kote duniani.

    "Tumepata usaidizi mkubwa sana kutoka kwa china katika swala hili la sayansi.mkataba huu utawasaidia wanasayansi kwa ubunifu ujuzi na elimunya juu ili kufikia upeo wetu"

    Baadhi ya wajumbe na wanasayansi waliohudhuria kongamano hili wametoa mwito wa wanafunzi kuzingatia masomo ya sayansi katika siku za baadae kwani bara hili linawahitaji zaidi kujitegemea kiuchumi na kutatua changamoto.

    "Niko hapa kama naibu mwenyekiti wa wanasayansi kutoka nchi za afrika mashariki,tumepiga hatua kubwa na sasa tutahakikisha tunapata wanasayansi wetu waliohitimu watakaozalisha fikra na ujuzi utakaotumika kimataifa"

    Bara la Afrika limetajwa kuwa na raslimali za thamani za miradi ya sayansi.

    Wanasayansi kutoka ,India,Quwait,Ghana,Burundi,Uganda ni miongoni mwa waliohudhuria na kupewa tuzo.

    Kongamano hili litaendelea kwa mda wa siku tatu na kutoa majibu ya maswali magumu yanayokabili maisha ya nchi zinazoendelea.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako