• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Unajua panya wanapenda sana kucheka?

  (GMT+08:00) 2016-11-16 10:29:15

  Watu wakitaja panya, hukumbuka mambo mabaya yakiwemo uchafu na tauni, na huwa na hofu moyoni. Lakini panya pia ni wanyama wa kupendeza, kwani wanapenda sana kucheka. Watatifi wa Chuo Kikuu cha Humboldt cha Ujerumani wamegundua ubongo wa panya una neva inayohusiana na vitendo vya kucheka.

  Watafiti Shimpei Ishiyama na Michael Brecht wamepima shughuli za neva husika kwenye ubongo wa panya, na kutafiti mabadiliko ya shughuli hizi kabla na baada ya kuwashwa. Utafiti unaonesha kuwa panya wakiwashwa, wanacheka sana na kucheza dansi kama waliofurahishwa, na inaonekana kwamba hata panya wanajua mikono ya binadamu itawawasha. Lakini vicheko vyao ni vya ultrasonic na havisikiki na binadamu. Kabla ya hapo wanasayansi walifikiri neva hizi zinahusiana na hisia ya kugusa tu, lakini utafiti huo mpya unaonesha kuwa neva hizi pia zinahusiana na hisia ya furaha.

  Watafiti pia wamejaribu kuchochea neva husika za panya badala ya kuwafanya wawashwe moja kwa moja. Majaribio yanaonesha kuwa neva hizi zikichochewa, panya pia wanacheka.

  Lakini panya wakiwa katika hali ya wasiwasi, kwa mfano, wakiwekwa kwenye mahali pa juu sana, kuwawasha au kuchochea neva zao hakutawachekesha. Wanasayansi wamesema jambo hili huenda linamaanisha kuwa mmoja akicheka baada ya kuwashwa, hakika ana furaha moyoni.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako