• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • WHO lalaani mashambulizi dhidi ya hospitali nchini Syria

    (GMT+08:00) 2016-11-17 10:21:53

    Shirika la afya duniani WHO limelaani mashambulizi yaliyotokea siku nne zilizopita dhidi ya hospitali tano nchini Syria, zikiwemo hospitali tatu magharibi mwa Aleppo na nyingine mbili mjini Idlib.

    Naibu msemaji wa Umoja wa Mataifa Bw. Farhan Haq amesema watu wawili wameuawa katika mashambulizi hayo, na wengine 19 walijeruhiwa wakiwemo wafanyakazi 6 wa afya.

    Mwaka huu WHO imerekodi mashambulizi 126 dhidi ya hospitali nchini Syria. Shirika hilo limezitaka pande zote husika ziheshimu usalama wa wafanyakazi wa afya, vituo vya afya, na vifaa vya matibabu. Bw Haq amesema inaonekana kuwa vituo vya afya nchini Syria vinashambuliwa kwa makusudi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako