• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wanaanga wa China kurejea duniani baada ya kumaliza majukumu yao kwenye anga ya juu

    (GMT+08:00) 2016-11-17 15:54:16

    Chombo cha anga za juu cha Shenzhou-11 kimejitenga na maabara ya anga za juu ya Tiangong-2, na kuanza safari ya kurejea duniani.

    Baada ya kujitenga, chomo hicho kitakuwa karibu na maabara hiyo mpaka watakapopata kibali kutoka kwa timu ya ardhini kuwaruhusu kuanza safari hiyo ya kurudi duniani.

    Wanaanga wawili walio ndani ya chombo hicho Jing Haipeng na Chen Dong, wameishi na kufanya kazi katika maabara hiyo kwa siku 30, ikiwa ni muda mrefu zaidi kwa wanaanga wa China kukaa kwenye anga ya juu. Wanaanga hao wameishukuru timu ya ardhini na kila mmoja ambaye anaunga mkono mradi wa China wa anga za juu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako