• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya yachukua hatua kukabiliana na ukame

    (GMT+08:00) 2016-11-18 09:22:01

    Serikali ya Kenya imechukua hatua za kukabiliana na ukame unaozikumba sehemu kadhaa nchini humo.

    Msemaji wa serikali ya nchi hiyo Bw. Eric Kiraithe amesema mpaka sasa mtu mmoja amethibithwa kufariki dunia kutokana na maafa hayo yanayoathiri kaunti 15 kati ya 47 nchini humo.

    Amesema, serikali za mitaa zimechukua hatua mbalimbali, ikiwemo uwekezaji mkubwa katika utoaji msaada wa chakula na maji safi, usimamizi wa magonjwa ya mifugo na uuzaji wa mifugo. Ameongeza kuwa fedha zaidi zimeidhinishwa na serikali kuu ili kukabiliana na maafa hayo.

    Kwa mujibu wa serikali ya Kenya, watu milioni 1.3 nchini humo wanahitaji msaada wa chakula kutokana na ukame huo unaokadiriwa kuendelea hadi mwaka kesho.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako