• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • FIFA yafungua kesi ya kuziadhibu Uingereza na Scotland kwa kukaidi sheria

    (GMT+08:00) 2016-11-18 09:40:48

    Bodi ya shirikisho la soka duniani, FIFA imetoa tamko la kufungua kesi juu ya taratibu za kinidhamu dhidi ya wachezaji wa timu mbili za Uingereza na Scotland baada ya timu hizo kuvaa vitambaa begani kama ishara ya maombolezo na kumbukumbu kwa wachezaji wenzao ambao walipoteza maisha vitani. FIFA imesisitiza kwamba kitendo kama hicho kinaangukia katika marufuku zifananazo na masuala ya kidini, masuala ya kisiasa ama kauli binafsi katika mechi za timu za taifa.

    Kwa pamoja timu ya Uingereza na Scotland ambazo ziko chini ya FIFA inaarifiwa kwamba wakati wa maadhimisho ya usiku wa ijumaa iliyopita za kufuzu Kombe la Dunia kwenye Uwanja wa Wembley kwamba walikuwa tayari wamejiandaa kukabiliana na matokeo ya kukaidi sheria za shirikisho la soka duniani FIFA. Mashirikisho yote mawili yanaweza kukabiliwa na faini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako