• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • "Uchumi wa Mikutano" wahimiza maendeleo ya uchumi

    (GMT+08:00) 2016-11-18 09:46:56

    Mkutano wa tatu wa Mtandao wa Internet duniani umefanyika leo mjini Wuzhen, mkoani Zhejiang. Huu ni moja kati ya mikutano mikubwa ya kimataifa iliyofanyika nchini China mwaka huu. Waraka wa Mkutano wa China uliochapishwa mwaka 2015 umeeleza kuwa, China inaandaa mikutano zaidi ya milioni 10 kila mwaka na kuleta faida ya kiuchumi zaidi ya yuan trilioni 1. Je, mikutano hiyo inaleta faida hizo kwa njia gani?

    Kwanza, "uchumi wa mikutano" unaweza kusaidia kuongeza ushawishi wa miji wenyeji wa mikutano hiyo, na kuhimiza mawasiliano na ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya miji hiyo na sehemu nyingine, pia inasukuma mbele maendeleo ya utalii, hoteli, mawasiliano, migahawa na mauzo ya rejareja katika miji hiyo. Kwa mfano, Wuzhen ambao ni mji mwenyeji wa Mkutano wa Mtandao wa Internet duniani, umewavutia wataalamu wa mtandao wa internet duniani na kupata uhai na nguvu mpya kutokana nao, faida hiyo pia imehimiza maendeleo ya uchumi ya huko pamoja na sehemu jirani.

    "Uchumi wa mikutano" ni msukumo wa maendeleo ya uchumi pia inaonesha kiwango cha maendeleo ya uchumi wa nchi. Mbali na kiwango cha juu cha uandaaji wa mikutano, mji mwenyeji wa mkutano pia unahitaji kuwa na mazingira mazuri ya kiasili, mawasiliano rahisi, na kiwango cha juu cha ufunguaji mlango kwa nje.

    Nairobi ni moja kati ya miji mikubwa ya kimataifa ambayo ina sifa hizo katika nchi za Afrika mashariki. Mwaka huu, Kenya imeandaa mikutano miwili ya kimataifa inayofuatiliwa na dunia nzima, nayo ni Mkutano wa Pili wa mazingira wa Umoja wa Mataifa uliofanyika mwezi Mei, na Mkutano wa 14 wa biashara na maendeleo wa Umoja wa Mataifa uliofanyika mwezi Julai. Mikutano hiyo iliwashirikisha watu zaidi ya elfu 10 kutoka nje ya nchi hiyo. Baada ya mikutano hiyo, washiriki walitembelea hifadhi za wanyama pori zinazojulikana duniani nchini humo, hivyo kuleta faida kubwa kwa mambo ya utalii nchini Kenya. Mkurugenzi wa Idara ya utalii ya Kenya alisema, Kenya imechukua kipande kimoja tu cha keki inayoletwa na "uchumi wa mikutano" wa Afrika ambayo inazidi kupanuka.

    Hali kadhalika kwa Tanzania. Dira ya Taifa 2025 imeweka 1engo la kukuza uchumi wa nchi kupitia diplomasia ya uchumi iliyo endelevu.

    Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ilifanikisha kufanyika makongamano na maonesho ya biashara na uwekezaji yaliyolenga kutangaza fursa za biashara na uwekezaji pamoja na vivutio vya utalii zilizopo Tanzania.

    Mbali na Kenya na Tanzania, nchi nyingine za Afrika zikiwemo Afrika Kusini, Zimbabwe, Zambia, Namibia na Ethiopia pia zinaandaa mikutano mbalimbali ya kimataifa kila mwaka, ili kuongeza ushawishi wao duniani na kuongeza ushiriki katika mambo ya kimataifa kwa kupitia "uchumi wa mikutano". Kutokana na mtizamo wa siku za baadae, "uchumi wa mikutano" barani Afrika utahimiza Afrika kuboresha ujenzi wa miundo mbili kama vile mawasiliano na upashanaji wa habari, ili kuhimiza maendeleo endelevu ya uchumi na jamii.

    Wachambuzi wanaona kuwa, "uchumi wa mikutano" duniani utadumisha wastani wa ongezeko la asilimia 4 katika miaka kadhaa ijayo. Inaaminika kuwa, kadiri ujenzi wa miundombinu na teknolojia ya upashanaji wa habari zinavyozidi kuboreshwa barani Afirka, ndivyo mikutano mingi zaidi ya kimataifa itakavyofanyika katika bara hilo, na Afrika inatazamiwa kunufaishwa zaidi kutokana na ongezeko la "uchumi wa mikutano"duniani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako