• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Ulaya wasema Tanzania ina haki ya kutosaini mkataba wa EPA

    (GMT+08:00) 2016-11-18 19:31:45

    Balozi wa Umoja wa Ulaya katika Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) Roeland Van de Geer amesema Tanzania ina haki ya kuamua kutosaini mkataba wa ushirikiano wa kibiashara na jumuiya ya Ulaya (EPA) hadi itakapojiridhisha manufaa yake.

    Akizunguma na waandishi wa habari, Van de Geer amesema ingawa Tanzania ina wasiwasi kuwa mkataba huo utadhoofisha juhudi za kufufua viwanda vyake, haoni kama kuna ushindani kwenye suala hilo hilo. Ameongeza kuwa ni vyema kwa nchi kuchukua muda kujiridhisha badala ya kukimbilia kusain bila kuangalia manufaa yake kwa raia wa nchi husika. Kauli hii inakuja miezi miwili tu baada ya mwenyekiti wa EAC, Rais John Magufuli kusema viongozi wa jumuiya hiyo wamekubaliana kupewa muda wa miezi mitatu ili Sekretarieti ya EAC iangalie na kupitia masharti ya EPA kabla ya kusaini ili kila mmoja afaidike.

    Hata hivyo, katika jumuiya hiyo ya EAC, nchi ambazo tayari zimesaini mkataba huo ni Kenya, Rwanda na Uganda huku Tanzania na Burundi zikiendelea kuchunguza faida kwa nchi zao. Rais Magufuli amesema katika kikao hicho, walibaini mambo 10 ambayo yanapaswa kuangaliwa kabla ya kufikia uamuzi kwa maslahi ya nchi na wananchi. Magufuli amesema mambo ya kuangaliwa kuwa ni jinsi gani nchi za EAC zitafaidika, njia gani itatumika kuzuia bidhaa za kilimo na kulinda wakulima, usawa, makusanyo yatokanayo na bidhaa zitakazoingizwa, Burundi itasainije huku ikiwa imewekewa vikwazo na EU, kujitoa kwa Uingereza EU na athari zake, kukosekana kipengele cha kuruhusu nchi nyingine kujihusisha na nchi za EAC kibiashara, kukosekana ushuru wa forodha na kipengele cha nchi kujitoa pale inapoona haijaridhika na mkataba huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako