• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa laeleza wasiwasi na kuibuka tena kwa vurugu za kikabila nchini Sudan Kusini

    (GMT+08:00) 2016-11-19 18:35:52

    Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeeleza wasiwasi wake kuhusu kuongezeka kwa vurugu za kikabila nchini Sudan Kusini na kulaani vikali mashambulizi dhidi ya raia, mauaji yanayolenga kabila fulani, kauli zenye chuki na uchochezi wa matumizi ya kimabavu.

    Kauli hizo zimo kwenye taarifa ya mkutano na waandishi wa habari iliyotolewa na Baraza la Usalama lenye nchi wajumbe 15 baada ya hotuba fupi aliyotoa mshauri maalumu wa Umoja wa Mataifa wa kuzuia mauaji ya kimbari Adama Dieng. Taarifa hiyo pia inasema wajumbe wa Baraza la Usalama wanatia wasiwasi na kuongezeka kwa mapigano ya kikabila nchini Sudan Kusini yaliyoripotiwa kufanywa na kundi la SPLA, upande wa upinzani wa SPLA, pamoja na wanamgambo na makundi yasiyojulikana yenye silaha.

    Bw. Dieng alimaliza ziara ya siku tatu nchini Sudan Kusini mapema wiki hii, ambapo aliionya nchi hiyo kuwa na hatari ya kukabiliwa na mauaji ya halaiki kama isipokuwa na hatua yoyote ya kutuliza hali ya sasa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako