• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yarudia wito wake wa kujenga FTAAP wakati maingiliano ya kiuchumi duniani yanayumbayumba

    (GMT+08:00) 2016-11-20 16:40:48

    China imerejea wito wake wa kusukuma mbele ujenzi wa Eneo la Biashara Huria la Asia na Pafisiki FTAAP wakati vitendo vya kujilinda vinazuia maingiliano ya kibiashara na kiuchumi ya kimataifa.

    Rais Xi Jinping wa China amesema kwenye hotuba yake aliyotoa kwenye Mkutano wa Viongozi wa Kiuchumi wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiuchumi ya Asia na Pasifiki APEC mjini Lima kwamba FTAAP ni mpango wa kimkakati ambao ni muhimu kwa mustakbali wa muda mrefu wa Asia na Pasifiki. Amewaambia viongozi wa kibiashara duniani kuwa China inatetea kwa uthabiti kuwa FTAAP ni utaratibu wa kitaasisi kwa ajili ya kuhakikisha uchumi wa wazi kwenye Asia na Pasifiki.

    Mkutano wa mwaka huu wa viongozi wa APEC unafanyika wakati uchumi wa dunia unafufuka taratibu na kukosa injini za ongezeko, pia kuna upinzani dhidi ya maingiliano ya kiuchumi ya kimataifa, biashara na uwekezaji hafifu pamoja na changamoto zinazoongezeka duniani ambazo pia zinaathiri mustakbali wa uchumi wa dunia.

    Xi ameongeza kuwa Asia na Pasifiki pia inakabiliwa na shinikizo linalofanana na kupambana na changamoto hizo kwa kuzidisha ushirikiano wa kiuchumi katika kanda hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako