• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ataka Mali kufanya uchaguzi wa serikali za mitaa kwa wakati uliopangwa

    (GMT+08:00) 2016-11-20 18:01:10

    Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Ban Ki-Moon ametoa mwito kwa pande mbalimbali za Mali kuhakikisha uchaguzi wa serikali za mitaa unafanyika bila matatizo.

    Bw. Moon, kwenye taarifa iliyotolewa kupitia msemaji wake, ametoa kauli hizo siku moja kabla ya serikali ya Mali kupanga kufanya uchaguzi wa serikali za mitaa Jumapili. Amesema kushindwa kutekelezwa kwa baadhi ya vifungu vilivyomo kwenye Makubaliano ya Amani na Mapatano ya Mali, na hali ya usalama ya kaskazini mwa Mali vinaweza kuathiri uchaguzi huo.

    Katibu mkuu huyo pia ameihimiza serikali ya Mali kufanya mazungumzo yanayojumuisha wadau mbalimbali, ili kuepusha vurugu kujitokeza kabla na baada ya uchaguzi huo, pia kuhakikisha uchaguzi huo unafanyika bila matatizo na mchakato wa kisiasa usirudi nyuma.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako