• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa APEC wa Lima wafungwa, na azimio lililofikiwa limesukuma mbele ujenzi wa eneo la biashara huria la kanda hiyo

    (GMT+08:00) 2016-11-21 16:29:43

    Mkutano usio rasmi wa viongozi wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiuchumi ya Asia na Pasifiki APEC umemalizika huko Lima, mji mkuu wa Peru, na "Azimio la Lima" lililopitishwa kwenye mkutano huo linaonesha kuwa pendekezo la China la kuanzisha eneo la biashara huria la Asia na Pasifiki limepiga hatua moja muhimu.

    Kwenye azimio hilo, makundi 21 ya kiuchumi katika kanda ya Asia na Pasifiki yamesisitiza kufanyika kwa juhudi za kufanikisha eneo la biashara huria la kanda hiyo, na kulifanya liwe njia kuu ya kuimarisha maingiliano ya kiuchumi. Viongozi wa makundi mbalimbali ya kiuchumi pia wameidhinisha ripoti ya utafiti wa kimkakati kuhusu eneo hilo iliyowasilishwa na mkutano wa mawaziri wa APEC na mapendekezo husika ya kisera.

    Rais Pedro Pablo Kuczynski wa Peru amesema baada ya kufungwa kwa mkutano huo kuwa, biashara ni msingi wa ustawi wa dunia, na China ni moja ya nguzo muhimu za kuhimiza maendeleo ya Asia na Pasifiki.

    Dira ya ujenzi wa eneo la biashara huria la Asia na Pasifiki ilitolewa kwenye mkutano wa APEC uliofanyika Vietnam mwaka 2006, na mkutano wa APEC wa Beijing uliofanyika mwaka 2014 ulifikia makubaliano kuhusu mpango wa APEC wa kujenga eneo hilo, kuzindua utafiti wa kimkakati wa jumla kuhusu masuala husika, na kusukuma mbele kwa pande zote mchakato wa eneo la biashara huria la Asia na Pasifiki.

    Mkutano wa mwaka huu wa APEC umefanyika wakati sera za kujilinda kibiashara na hasira za kupinga utandawazi vinaibuka duniani. Akitoa hotuba kwenye mkutano huo, rais Xi Jinping wa China amesisitiza uthabiti wa kuhimiza utandawazi duniani, kufanya uchumi wa dunia uwe jumuishi na wenye manufaa kwa wote, na pia kupinga aina zote za vitendo vya kujilinda kibiashara.

    Rais Xi pia amesema tangu China ilipojiunga na Jumuiya ya APEC miaka 25 iliyopita, siku zote inatilia maanani kufungua mlango kwanza kwa Asia na Pasifiki, na inapenda kushirikiana na pande mbalimbali, kuweka kipaumbele maendeleo, kupanua ufunguaji mlango, kuhimiza maingiliano ya kiuchumi na ujenzi wa miundombinu, na kuimarisha ushirikiano katika kanda ya Asia na Pasifiki.

    Viongozi wa makundi mbalimbali ya kiuchumi ya APEC wamesema Asia na Pasifiki ni injini muhimu ya ukuaji wa uchumi wa dunia, na makundi hayo yanapaswa kuendelea kutumia ipasavyo Jumuiya ya APEC, kutekeleza vizuri mafanikio yaliyopatikana kwenye mikutano iliyopita, na kupanga mustakbali wa ushirikiano wa Asia na Pasifiki, ili kukuza zaidi uchumi wa kanda hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako