• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa alaani mashambulizi dhidi ya raia nchini Syria

    (GMT+08:00) 2016-11-21 18:53:58

    Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Ban Ki-moon amelaani mashambulizi yanayotokea mara kwa mara nchini Syria na kusababisha vifo na majeruhi kwa raia wengi.

    Taarifa iliyotolewa na msemaji wa katibu mkuu huyo imesema hakuna hospitali yoyote inayompokea mgonjwa mashariki mwa Aleppo, mji uliopo kaskazini mwa Syria, na pia imelaani mashambulizi yaliyolenga shule na kusababisha vifo vya wanafunzi.

    Habari nyingine zinasema, mjumbe maalum wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia suala la Syria Bw.Staffan de Mistura amesema, kuna tofauti ya maoni kati yake na serikali ya Syria kuhusu utatuzi wa hali ya mji wa Aleppo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako