• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Binadamu akisema uwongo, pua inakuwa imoto zaidi

    (GMT+08:00) 2016-11-22 19:00:00

    Unamjua Pinocchio? Hadithi iliyoandikwa na mwandishi wa habari wa Italia Carlo Collodi katika mwaka 1881 hadi 1883 inasema seremala mzee alitengeneza mwanasesere hai kama mtoto halisi, na kumpa jina la Pinocchio. Lakini Pinocchio alipata tabia nyingi mbaya, ikiwemo tabia ya kusema uwongo. Lakini akisema uwongo, pua yake inakuwa refu sana.

    Hivi karibuni wanasayansi wa kitivo cha saikolojia cha Chuo Kikuu cha Granada cha Hispania wamegundua kuwa watu wanaposema uwongo, huwa inatokea hali inayofanana na kwenye hadithi ya Pinocchio, yaani pua zao zinakuwa zimoto zaidi. Hii ni mara ya kwanza kwa wanasayansi kupima joto wanapotafiti suala la kisaikolojia, na wamegundua jambo hili la kuchekesha.

    Licha ya kuongezeka kwa joto kwenye pua, misuli ndani ya macho pia inakuwa imoto zaidi, na sehemu iitwayo Insular cortex kwenye ubongo pia inaanza kufanya kazi. Insular cortex inadhibiti hisia za binadamu, pia inahusiana na joto la mwili.

    Mambo mengine pia yatasababisha mabadiliko ya joto mwilini. Wanasayansi wamegundua kuwa watu wanapofanya kazi ambayo inawahitaji kufikiri, nyuso zao zinakuwa baridi zaidi, na wanapokuwa na wasiwasi, nyuso zao zinakuwa zimoto.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako