• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Nyota wa zamani wa kikapu nchini Marekani Dennis Rodman ashtakiwa kwa kugonga na kutoroka

    (GMT+08:00) 2016-11-23 14:32:16

    Aliyekuwa nyota wa mpira wa kikapu nchini Marekani Dennis Rodman ameshtakiwa kwa kosa la kugonga na kutoroka ambalo hukumu yake ni kifungo kisichozidi miaka miwili.

    Nyota huyo aliye na umri wa miaka 55 anatuhumiwa kwa kuendesha gari kwa kutumia barabara isiofaa huko kusini mwa jimbo la California, swala lililolazimu gari jingine kukwepa na kugonga ukuta. Waendesha mashtaka wanadai kwamba Rodman baadaye alitoroka eneo hilo Julai 20 na kuwapa maafisa wa polisi habari za uongo.

    Pia ameshtakiwa kwa kuendesha gari bila leseni. Wakili wa Rodman, Paul Meyer anasema ajali hiyo ilitokea katika eneo ambalo halina ishara za trafiki zinazoonekana na kwamba alijitahidi kuzuia ajali hiyo kwa kutogonganisha, kusimama na kuzungumza na watu waliokuwa ndani ya gari hilo. Kesi hiyo inatarajiwa kuendelea Januari 20.

    Rodman alishinda mataji mawili akiwa na klabu ya Detroit Pistons pamoja na timu maarufu ya Chicago Bulls katika miaka ya 90 akishirikiana na Michael Jordan.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako