• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China na Afrika Kusini zakubaliana maeneo matano muhimu ya ushirikiano

    (GMT+08:00) 2016-11-23 18:23:35

    China na Afrika Kusini zimekubaliana kuongeza ushirikiano katika maeneo matano muhimu yakiwemo kisiasa, kiuchumi na kibiashara pamoja na mawasiliano ya watu wa pande hizo mbili.

    Makubaliano hayo yamefikiwa katika kikao cha sita cha Tume ya China na Afrika Kusini, ambacho kiliongozwa kwa pamoja na makamu wa rais wa China Li Yuanchao na makamu wa rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa.

    Pande hizo mbili zimekubaliana kuimarisha uaminifu wa kisiasa kwa kudumisha kasi ya mawasiliano ya ngazi ya juu na kuendelea kuunga mkono na kufanya uratibu kwa pamoja kuhusu masuala yanayohusu maslahi muhimu na masuala yanayofuatiliwa na pande hizo mbili. Pia nchi hizo zimekubaliana kuongeza ushirikiano katika maeneo mengine ikiwemo ujenzi wa miundombinu, maendeleo ya maeneo maalum ya ukanda wa kiuchumi na viwanda, utengenezaji wa vifaa, na uchumi wa baharini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako