• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China ataka ushawishi mkubwa wa vyombo vya habari ili kuonesha sura halisi ya China na nchi za Latin Amerika

    (GMT+08:00) 2016-11-23 18:27:30

    Rais Xi Jinping wa China ambaye yupo ziarani nchini Chile alihudhuria ufunguzi wa mkutano wa wakuu wa vyombo vya habari vya China na Latin Amerika jana mjini Santiago. Kwenye hotuba yake, rais Xi ametaka vyombo vya habari vya China na Latin Amerika kushirikiana kupanua ushawishi wao ili kuonesha sura halisi ya China na Latin Amerika kwa dunia nzima.

    Akizungumza kwenye mkutano wa wakuu wa vyombo vya habari vya China na Latina America uliofanyika mjini Santiago, Chile, Rais Xi, akiwa na mwenyeji wake rais Michelle Bachelet wa Chile, amesema mawasiliano ya vyombo vya habari ni sehemu muhimu ya uhusiano kati ya China na Latin Amerika, na vyombo vya habari vya pande hizo mbili vinaweza kufanya kazi zaidi ili kuenzi na kuongeza urafiki kati ya watu wao.

    Rais Xi pia amekumbusha kuwa vyombo vya habari vya China na Latin Amerika vinapaswa kujihusisha kwenye masuala makuu kama vile amani na maendeleo ya dunia.

    Wakati huohuo, mkuu wa Radio China Kimataifa CRI Bw. Wang Gengnian naye pia ametoa hotuba akitoa wito kwa vyombo vya habari vya China na Latin Amerika kuimarisha ushirikiano wao ili watu wa pande hizo mbili waelewane zaidi na kuchangia ushirikiano kati ya pande hizo mbili.

    Bw. Wang amesema vyombo vya habari ni jukwaa la mawasiliano na njia za kujifunza aina tofauti za ustaarabu kati ya watu wa China na Latin Amerika, pia ni daraja linalowaunganisha watu hao. Hivi sasa ushirikiano kati ya vyombo vya habari vya pande hizo unaendelezwa vizuri, na inatarajiwa kuwa wigo wa ushirikiano huo unapanuliwa zaidi ili kujenga mustakbali mzuri na kupata mafanikio zaidi.

    Wang pia amesema vyombo vya habari vya China na Latin Amerika vinapaswa kuongeza nguvu za kutunga mada kwenye masuala yanayohusu maslahi makuu ya pande hizo mbili, kutoa sauti moja, ili kuongeza ushawishi wao katika masuala ya kikanda na kimataifa, pia kuhimiza ujenzi wa utaratibu mpya wa vyombo vya habari vya kimataifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako