Bruce Arena, ameteuliwa kuwa meneja mkuu wa timu ya taifa ya Marekani kwa mara ya pili, na kumrithi Jurgen Klinsmann aliyetimuliwa siku ya Jumatatu. Mmarekani huyo mwenye umri wa miaka 65, ambaye ameiacha timu ya LA Galaxy, na kuchukua nafasi hiyo, aliongoza nchi yake mwaka 2002 hatua ya robo fainali alipoanza kuifundisha kwa mara ya kwanza.
Arena pia aliongeza kiwango cha ushindi kati ya mameneja wa Marekani, kwa kupata ushindi mara 71 kati ya michezo 130 katika miaka ya 1998 na 2006. Pia ameshinda vikombe vitano katika ligi ya MSL akiiongoza timu ya LA Galaxy ya jiji la New York na DC United.
Marekani wamo katika nafasi ya mwisho ya nchi sita zinazoshindania kufuzu Kombe la Dunia kutoka bara la Amerika, nyuma ya mataifa madogo kama vile Panama na Honduras. Arena atachukua hatamu ya kuwa meneja tarehe 1 mwezi Disemba, na mechi yake ya kwanza itakuwa nyumbani dhidi ya Honduras tarehe 24 Machi mwaka 2017.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |