• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uwekezaji wa makampuni ya China nje ya nchi umeingia kwenye "kipindi cha dhahabu"

    (GMT+08:00) 2016-11-24 19:28:32

    Ripoti mpya iliyotolewa na Kituo cha China na Utandawazi CCG imesema, uwekezaji wa makampuni ya China nje ya nchi umeingia kwenye "kipindi cha dhahabu" wakati kunaibuka pingamizi dhidi ya utandawazi duniani.

    Ripoti hiyo kuhusu makampuni ya China kufanya biashara na nchi za nje inasema uwekezaji wa China nje ya nchi umeongezeka kwa miaka kumi mfuluilizo toka mwaka 2005, na kufikia dola za kimarekani bilioni 145.67 mwaka jana. Ripoti hiyo pia inaona kuwa uwekezaji wa moja kwa moja wa kimataifa nje ya nchi umefufuka kwa nguvu na kufikia kiwango cha juu zaidi baada ya kutokea kwa msukosuko wa kifedha duniani mwaka 2009.

    Hata hivyo hivi karibuni mwelekeo wa kuibuka kwa sera za kujilinda kibiashara unaonekana kwenye baadhi ya nchi, na kujitoa kwa Uingereza kwenye Umoja wa Ulaya na kauli za rais mteule wa Marekani Donald Trump vimeongeza makali ya kupinga utandawazi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako