• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Ulaya kutoa zaidi ya dola za Kimarekani milioni 170 kusaidia mageuzi nchini Ukraine

    (GMT+08:00) 2016-11-25 18:49:28

    Mkutano wa kilele wa Umoja wa Ulaya na Ukraine uliofanyika mjini Brussels umeamua kutoa Euro milioni 170, sawa na dola za Marekani miloni 179.7 kuunga mkono mageuzi nchini Ukraine.

    Kamati ya Umoja huo imesema, Euro milioni 15 zitatumika kupambana na rushwa, Euro miloni 104 kwa ajili ya mageuzi ya utawala na Euro milioni 52.5 katika kuhimiza utawala wa sheria.

    Wakati huohuo, Umoja huo pia umesaini makubaliano na Ukraine kuhusu kupanua ushirikiano kwene ufanisi wa matumizi ya nishati na nishati endelevu. Pia Umoja wa Ulaya utawaruhusu raia wa Ukraine kuingia kwenye nchi za Umoja huo bila ya viza ifakapo mwishoni mwa mwaka huu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako