• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kiongozi wa zamani wa Cuba Fidel Castro afariki dunia

    (GMT+08:00) 2016-11-26 15:35:01

    Kiongozi wa zamani na mwanamapinduzi wa Cuba Fidel Castro amefariki dunia.

    Akitangaza kupitia televisheni ya Taifa kiongozi wa Cuba Raul Castro amesema, amiri jeshi mkuu wa mapinduzi ya Cuba amefariki dunia saa nne na dakika 29 usiku wa kuamkia leo.

    Mkongwe huyo wa mapinduzi amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 90 ambapo mara ya mwisho alionekana hadharani mwezi Agosti.

    Fidel Castro aliongoza Cuba chini ya chama kimoja kwa takribani nusu karne kabla ya kukabidhi madaraka kwa mdogo wake Raul mnamo mwaka 2008 kutokana na afya yake kuwa mbaya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako